Honda atibua ushindi wa Senegar dhidi ya Japan, Uingereza yaua Panama

Goli la kusawazisha lililofungwa kunako dakika ya 78 na mchezaji aliyeingia kipindi cha pili Honda limetibuasherehe za ushindi kwa Senegar baada ya kutoka sare na Japan mabao 2-2 usiku huu kombe la dunia Urusi.

Senegar ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Sadio Mane dakika ya 11 kabla ya Inui hajaisawazishia Japan, Senegar walipata bao la pili kupitia kwa Wague dakika ya 70 lakini Honda akachomoa na kuwa 2-2 timu zote sasa zinakbana koo kileleni zote zikiwa na pointi 4.

Jioni ya leo Uingereza imsichapa Panama mabao 6-1 uwanja wa Stadion Nizhny Novgorrod,mabao matatu pekee yamefungwa na Harry Kane dakika za 22, 45 na 62 yote kwa penalti, mengine John Stones dakika ya 8 na 40 na lingine limefungwa na Jesse Lingard dakika ya 36 na lile la Panama limefungwa na Felipe Baloy  dakika ya 78, usiku wa saa 3 Poland itaumana na Colombia

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA