UFARANSA YATANGULIA 16 BORA IKIIBANJUA PERU 1-0, DENMARK IKISHIKWA SHATI NA AUSTRALIA, MESSI ASUBIRIWA NA CROATIA

Mabingwa wa dunia wa mwaka 1998 Ufaransa wametangulia hatua ya 16 bora ya kombe la dunia kundi C baada ya jioni ya leo kuilaza Peru bao 1-0 katika uwanja wa Ekateringburg Arena nchini Urusi.

Goli ambalo limeibeba Ufaransa lilifungwa na kinda Kylian Mbappe dakika ya 34, hata hivyo Mbappe ameingia kwenye rekodi ya kufunga goli katika fainali hizo akiwa na umri mdogo, Mbappe ana miaka 19.

Katika mchezo mwingine ulioanza saa tisa alasiri, Denmark imebanwa mbavu na Australia baada kutoka sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Samara, goli la Denmark lilifungwa na Christian Eriksen dakika ya 7 na la kusawazisha la Peru lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Mile Jedinak hasa baada ya mchezaji mwenye asili ya Tanzania Yusuf Poulsen kuushika mpira, goli hilo kilifungwa dakika ya 38.

Hata hivyo Mtanzania huyo alipewa kadi nyekundu,mchezo mwingine wa kundi D unataraji kupigwa katika uwanja wa Nizhni Novgorod kati ya Argentina na Croatia mechi ambayo itakuwa ni ya maonyesho kwa Lionel Messi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA