Akina Honda waivua ubingwa Ujerumani

Ujerumani imevuliwa ubingwa wa kombe la dunia leo baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Korea Kusini katika mchezo wa kundi F uwanja wa Kazan Arena, Urusi.

Mabao ya Korea Kusini yamefungwa na Kim Young Gwon dakika ya 90 za kawaida lingine Son Heung Min dakika sita za nyongeza na kusababisha Ujerumani kuvuliwa taji lake ililolitwaa mwaka 2014 nchini Brazil baada ya kuilaza Argentina 1-0 katika fainali.

Pia Ujwrumani inakuwa imetolewa kwa mara ya kwanza kuanzia hatua ya makundi baada ya miaka 80, Ujerumani na Korea Kusini zote zimeaga mashindano hayo na kuzipisha Sweden na Mexico kutinga hatua ya 16 bora.

Sweden nayo imeichapa Mexico mabao 3-0 yaliyofungwa na LudwigAugustinsson dakika ya 50, Andreas Grangvist kwa penalti dakika ya 52 na Edson Alvarez aliyejifunga mwenyewe dakika ya 74, usiku huu Brazil inaumana na Serbia wakati Colombia inaumana na Costa Rica

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA