DIEGO COSTA AIPA USHINDI WA KWANZA HISPANIA DHIDI YA IRAN
Goli pekee laushindi lililofungwa dakika ya 54 na mshambuliaji Diego Costa leo usiku limetoshakuwapa ushindi wa kwanza kundi B timu ya taifa ya Hidpania wa bao 1-0 dhidi ya Iran mchezo wa kombe la dunia uliopigwa uwanja wa Kazan Arena.
Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafungana hata bao, vijana wa Iran walionekana kuwamudu vema Hispania wenye nyota mbalimbali wanaocheza vilabu vikubwa barani Ulaya.
Na kama si mwamuzi wa mchezo huo kulikataa goli la Iran huenda mchezo huo ungemalizika kwa sare na kuiweka Hispania taabani, sasa vita ya kuwania kuingia hatua ya 16 bora ni kati ya Ureno, Hispania na Iran ambapo mechi zao za mwisho zitaamua