Brazil na Serbia ni roho mkononi, Ujerumani na Korea Kusini kazi ipo
Huenda historia ikajirudia kwa miamba Brazil kukutana tena na Ujerumani kwenye hatua ya mtoano ya 16 bora iwapo leo hii miamba hiyo itakapofanikiwa kutinga hatua hiyo.
Katika kundi E Brazil inaumana na Serbia uwanja wa Spartak mjini Moscow na Uswisi itaumana na Costa Rica uwanja wa Nizhni Novgorod Arena.
Nafasi bado ngumu kwa Brazil kwani Serbia na Uswisi nao wana nafasi ya kutinga 16 bora. Vita nyingine ipo kundi F wakati mabingwa watetezi Ujerumani wakiumana na Korea Kusini uwanja wa Kazan Stadium hiyo itakuwa saa 3 usiku na pia Mexico itaumana na Sweden, pia nafasi ni ngumu kwa Ujerumani kufuzu hatua ya 16 bora kwani hata Sweden ina nafasi, tayari Mexico imeshafuzu 16 bora