Argentina yajipigia Nigeria, Croatia yawa mbabe kundi D
Magoli mawili yaliyofungwa na Lionel Messi dakika ya 14 na Marcos Rojo dakika ya 86 yametosha kabisa kuipa ushindi Argentina na kutinga hatua ya 16 bora kombe la dunia kundi D uwanja aa Saint Petersburg mjini Moscow baada ya kuifunga Nigeria mabao 2-1.
Bao la Nigeria la kufuta machozi lilifungwa na Victor Moses kwa mkwaju wa penalti dakika ya 51, Nigeria imetupwa nje ya mashindano hayo.
Croatia nayo imeibuka mbabe kundi D baada ya kuilaza Iceland mabao 2-1 uwanja wa Roston On Don Arena, mabao ya Croatia yamefungwa na Milan Badelj dakika ya 53 na Ivan Perisic dakika ya 90 na lile la Iceland lilifungwa na Gylfi Sigurdsson dakika ya 76 kwa mkwaju wa penalti
Croatia wanamaliza mechi zote tatu wakiibuka wababe baada ya pia kuzishinda Nigeria na Argentina na kufikisha alama 9