NIGERIA YAFUFUA MATUMAINI YA WAAFRIKA, BRAZIL YAANZA NA MOTO
Timu ya taifa ya Nigeria imefufua matumaini ya kutinga hatua ya mtoano baada ya kuichapa Iceland mabao 2-0 na kuifanya ifikishe pointi tatu ikihitaji sare katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Argentina.
Mabao yote ya Nigeria yamewekwa kimiani na mshambuliaji wake Ahmed Musa kunako dakika ya 49 na 75. Nayo Brazil ilifufua kasi yake baada ya kuichapa Costa Rica mabao 2-0 mchezo ukipigwa uwanja wa Saint Petersburg.
Alianza Philipe Coutinho kuifungia Brazil bao la kuongoza dakika ya 90 kabla ya Neymar Dos Santos kufunga la pili katika dakika saba za nyongeza, kwa matokeo hayo Brazil inafikisha pointi nne, mchezp mwingine leo unatarajia kuanza saa tatu kati ya Uswisi na Serbia