TIMU ZA TANZANIA ZAANZA KWA KISHINDO KAGAME CUP
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame zimeanza vema baada ya leo Azam Fc na Singida United kila moja kutoka na ushindi.
Mechi ya kwanza ilianza kwa wawakilishi wa Zanzibar, timu ya JKU ikianza kwa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa kundi A uliopigwa uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam, mchezo huo ulipigwa saa nane mchana.
Baadaye saa 10 jioni mabingwa watetezi Azam Fc ilianza vema kampeni yake baada ya kuilaza Kator ya Sudan mabao 2-1, magoli yote ya Azam yamefungwa na Shaaban Iddi Chilunda.
Usiku huu Singida United imeanza vema michuano hiyo baada ya kuilaza APR ya Rwanda mabao 2-1, magoli ya Singida United yamefungwa na Habibu Kyombo dakika ya 7 na Tibar John dakika ya 82 wakati lile la APR limefungwa na Akizimana Muhadji.
Singida United sasa inaongoza kundi C lenye timu za Simba na Dakadaha ya Somalia ambazo kesho zinaumana saa 8:00 mchana katika uwanja wa Taifa