Ronaldo kuendeleza moto kwa Morocco leo, Hispania na Iran ngoma inogile
Raundi ya pili ya kombe la dunia inaendelea leo baada ya jana Misri na wenyeji Urusikucheza mechi zao za pili, mitanange leo itakuwa mitatu ambapp Uruguay iraanza kwa kuumana na Saudi Arabia katika mchezo wa kundi A uwanja wa Rostov Arena.
Lakini baadaye Ureno yenye staa wake mahiri duniani Cristiano Rondo yenyewe itashuka dimbani kuwavaa wawakilishi wengine wa Afrika,Morocco katika uwanja wa Luzhniki Arena jijini Noscow, Ronaldo anaongoza kwa magoli akifunga matatu na leo anataka kuendeleza tena rekodi yake ya kutupia.
Hispania nayo inaumana na watengeneza nyuklia wa Iran mechi ambayo itakuwa kali na ya kusisimua kutokana na historia ya mataifa hayo wawili kuhusiana kindugu tokea karne zilizopita