Singida United yachukua nafasi ya Yanga kombe la Kagame

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Timu ya Singida United ya mkoani Singida imepewa nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame baada ya Yanga Sc kujitoa katika kinyang' anyiro hicho.

Katibu mkuu wa CECAFA Nicholaus Musonye amesema Singida United itashiriki michuano hiyo na imepangwa kundi C walilokuwa Yanga Sc ambao wamejiondoa, Yanga wamejitoa kwa sababu wana mchezo wao wa kombe la Shirikisho barani Afrika na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia hivyo wameshindwa kushirikimichuao hiyo.

Singida United itaanza kwa kucheza na APR katika uwanja wa Azam Complex Chamazi na kundi lao linahusisha timu nne ambazo ni Simba Sc,  Dakadaha ya Somalia na APR ya Uganda

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI