Senegar yaibeba Afrika kwa kuilaza Poland, Japan nayo hakuna kulala
Wawakilishi wa bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia nchini Urusi, Senegar imeanza vema baada ya kuichapa Poland mabao 2-1 katika mchezo wa kundi H uwanja wa Spartak jijini Moscow.
Poland walijikuta wanafungwa bao dakika ya 37 na Thiago Cionek kabla ya Niang kufunga la pili dakika ya 60 na dakika ya 86 Grzegorz Krychowiak akaifungia bao la kufutia machozi timu yake ya Poland, hayo ni matokeo mazuri kwa Senegar kwanj imekuwa timu ya kwanza kwa Afrika kushinda.
Mchana timu ya taifa ya Japan imeilaza Colombia mabao 2-1 yaliyofungwa na Shinji Kagawa dakika ya 6 na Yuya Osako dakika ya 73 kabla ya Juan Fernando Quintero kufunga la kufutia machozi kwa upande wa Colombia kunako dakika ya 39, mchezo ulifanyika katika uwanja wa Saransk, usiku huu wenyeji Urusi wanaumana na Misri