Salamba afungua akaunti ya mabao, Simba ikiifumua Dakadaha 4-0
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mabingwa wa Tanzania bara Simba Sc mchana wa leo imeanza vema michuano ya kombe la Kagame baada ya kuilaza Dakadaha ya Somalia mabao 4-0 mchezo wa kundi C uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kukamata usukani wa kundi hilo.
Ikichezesha karibu wachezaji wake wapya iliowasajili hivi karibuni kama Paschal Wawa, Adam Salamba na wengineo ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Marcel Kaheza aliyesajiliwa kutoka Majimaji ya Songea dakika ya 14 kabla ya Adam Salamba kufunga la pili dakika ya 23.
Dakadaha hawakuonyesha ushindani wowote wakajikuta wanapigwa la tatu dakika ya 45 likifungwa na Rashid Juma, Simba iliandika bao la nne lililofungwa tena naSalamba dakika ya 76 na kufanya iibuke na ushindi huo mnono