MTIBWA SUGAR YAIBOMOA KAGERA SUGAR
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imeibomoa Kagera Sugar baada ya kumnasa kiungo mshambuliaji Jaffar Kibay kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili.
Usajili huo ni sehemu ya kukiimarisha kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao pia ni matayarisho yake kwa ajili ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.
Akizungumzia usajili huo Afisa habari wa Mtibwa Sugar, Tobias Kifaru amesema ujio wa Kibaya ndani ya kikosi hicho ni kama amerejea tena nyumbani kwani aliwahi kuichezea Mtibwa kabla hajajiunga na Kagera Sugar