AFRIKA FUNGU LA KUKOSA KOMBE LA DUNIA, SENEGAR YAAGA KWA KICHAPO
Bara la Afrika limeshindwa kuingiza hata timu moja katika hatua ya 16 bora ya kombe la dunia nchini Urusi baada ya wawakilishi wake watano wote kuaga katika hatua ya makundi.
Senegar ambao pekee ndio waliokuwa wakipewa nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano imechapwa bao 1-0 uwanja wa Samara Arena Urusi mchezo wa kundi H.
Bao ambalo limeitupa nje Senegar limefungwa na beki Yerry Mina dakika ya 74, Senegar sasa inaungana na Poland kuyaaga mashindano hayo licha kwamba nayo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Japan, mataifa ya Afrika ambayo nayo yametolewa ni Misri, Morocco, Nigeria na Tunisia