Kimenuka, Leonarda na Sony Lava wamwagana

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba video vixen Leonarda Wolper na mwimbaji na mtunzi wa mashairi Sebastian "Sony Lava" ambao walikuwa wakiishi pamoja kama mke na mume hatimaye wamwagana.

Leonarda Wolper amesema jana kwamba ameamua kuachana na Sony Lava ambaye hivi karibuni alitambulisha video yake ya "Na wewe"  aliyomshirikisha Leonarda katika video kwa madai amekuwa akimtangaza vibaya kwa watu.

Leonarda amesema kwamba Sony Lava amekuwa akijisifu kwa marafiki zake kuwa yeye ni mke wake kitu ambacho si kweli, "Mimi na Sony Lava ni marafiki tu na wala siyo wapenzi kama anavyojitamba, siwezi kutoka naye hata mara moja namchukulia kama kaka yangu". alisema Leonarda.

Alipoulizwa Sony Lava kuhusu kuachana na Leonarda akakiri ni kweli wameachana lakini alidai alikuwa mkewe na si rafiki kama anavyosema, "Leonarda ni kama mke wangu tumeishi wote zaidi ya mwaka sasa lakini ushamba ndio uliomfanya tuachane, ana mambo ya kushobokea watu", alisema Sony Lava ambaye sasa anatamba na wimbo wake "Na wewe" katika media mbalimbali

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA