KAGERE ATUA KUMALIZANA NA SIMBA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba Sc hawatanii kwenye masuala ya usajili baada ya kufanikiwa kumshusha mazoezini Muivory Coast, Paschal Wawa Serge ambaye pia alikuwa akitakiwa na mahasimu wao Yanga, Simba wamemleta straika wa Gor Mahia ya Kenya, Mnyarwanda Meddie Kagere.
Kahere alitua nchini jana tayari kabisa kwa ajili ya mazungumzo na Simba na mambo yakienda vizuri anamwaga wino kuitumikia klabu hiyo katika michuano mbalimbali msimu ujao.
Kagere ameambatana na wakala wake na mipango ikienda sawia basi atavaa jezi za rangi nyekundu na nyeupe zinazovaliwa na klabu hiyo, Kagere alikuwa akitajwa pia kujiunga na Yanga, lakini Yanga wameshindwa kutoa milioni 180 alizokuwa akihitaji nyota huyo, Mohamed "Mo" Dewji ameamua kumleta ili kumsainisha, pia Simba inaweza kumalizana na straika Victor Patrick kutoka Nigeria