SIMBA YAMSHUSHA WAWA MAZOEZINI, KUCHEZA KAGAME

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Simba Sc wameifanyia unyamamkubwa Yanga Sc ambap ni mahasimu wao wa jadi baada ya kuwazunguka kwa nyuma na kumnasa beki kisiki wa El Merreikh ya Sudan ambaye aliwahi kucheza katika klabu ya Azam Fc, Paschal Wawa Serge raia wa Ivory Coast.

Beki huyo amewasili nchini na leo amehudhuria mazoezi ya klabu hiyo Boko Veterani, Wawa ameungana nawacjezaji wenzake na taarifa zinasema kuwa atatumika katika michuano ya Klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu Kagame Cup na akiwini atapewa mkataba.

Beki huyo ilikuwa asajiliwe na Yanga lakini wameshindwa kunleta nchini na wenzao wamefanikiwa kumleta na inasemekana atasaini mkataba wa miaka miwili, nafasi ya Wawa ni ya Laudit Mavugo ambaye anajiunga na KMC au Mbao Fc

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA