Chirwa mambo safi Yanga
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Kamati ya nidhamu, sheria na haki za wachezaji ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) imemaliza utata uliokuwa ukiwaandama wachezaji wa Yanga, Obrey Chirwa raia wa Zambia na Simon Msuva ambao walisimamishwa kutokana na makosa waliyofanya msimu uliopita. Nyota hao wawili walisimamishwa kucheza Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu baada ya kudaiwa kumsukuma mwamuzi aliochezesha mechi kati ya Yanga na Mbao FC mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara. Msuva yeye tayari ameshaachana na Yanga ambapo amesajiliwa na Difaa El Jajida ya Morocco wakati Chirwa bado anakipiga Yanga na amekosa mechi mbili moja ikiwa ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na nyingine ya Ligi Kuu Bara. Lakini leo hii kamati hiyo imetangaza kuwaachia huru nyota hao, kwa maana hiyo Chirwa sasa ataichezea Yanga katika mechi zijazo za Ligi Kuu Bara wakati Msuva ataitumikia timu ya taifa, Taifa Stars ambayo mwishoni mwa wiki itacheza na Botswana mchezo unaotambuliwa na Fifa Obrey Chirwa yuko huru sas...