Mwambusi atajwa kurejea Mbeya City
Na Exipedito Mataruma. Mbeya
Aliyekuwa kocha msaidizi wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC, Juma Mwambusi anahusishwa kurejea timu yake ya zamani ya Mbeya City kama kocha mkuu kuchukua nafasi ya Mmalawi Kinah Phiri.
Taarifa ambazo zimezagaa jijini Mbeya zinasema mazungumzo kati ya Mwambusi na viongozi wa Mbeya City yanaendelea vizuri na kila dalili zinaonekana kocha huyo aliyeipa mafanikio makubwa timu hiyo anarejea kazini.
Lakini Mwambusi ameweka sharti la kupumzika kwa sasa kama alivyotamka awali wakati akiwaaga Wanayanga kwamba anaachana na klabu hiyo aliyoitumikia kwa misimu miwili yote akiisaidia kutwaa ubingwa wa Bara.
Mwambusi huenda akaanza kukinoa kikosi hicho katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, kocha huyo pia amewahi kuinoa Tanzania Prisons pia ya jijini Mbeya