AJIBU AWATUMIA SALAMU SIMBA
Na Mwandishi Wetu. Pemba
Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara Yanga SC imeifunga timu ya Chipukizi ya Wete Pemba bao 1-0 mchezo wa kirafiki uliofanyika katika Uwanja wa Gombani mjini hapa.
Mabingwa hao wa Bara wametua Pemba tangu majuzi wakitokea Dar es Salaam wakipitia Unguja ambapo waliweza kucheza na Mlandege na kushinda mabao 2-0, na ujio wao Pemba ni kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Simba jumatano ijayo kuwania Ngao ya Jamii uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Vijana hao wa Yanga wamecheza mpira mzuri na kuwazidi maarifa Chipukizi ambao nao walionyesha kuwamudu Yanga lakini mshambuliaji Ibrahim Ajibu Migomba akaifungia Yanga bao pekee la ushindi ambalo ni kama salamu kwa timu yake ya zamani Simba ambao watakutana Jumatano ijayo