SOPHIA KIBENA ALIACHA SHULE KISA MIMBA

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Agizo la Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli la kuzuia wasichana wanaopata mimba mashuleni kutoendelea tena na masomo kama wadau wa elimu walivyotaka waendelee, msanii wa filamu anayekuja juu kwa sasa, Sophia Abdul Kinyogoli "Kibena" amesema hata yeye yalimkuta.

Akizungumza na Mambo Uwanjani, Kibena amesema alilazimika kukatisha masomo ya sekondari kidato cha pili kwakuwa alipewa ujauzito, anasema ujauzito huo alipewa na mume wa mtu na hatosahau kwa kuacha masomo kwani huenda sasa hivi angekuwa mbali.

Kibena kwa sasa anafanya vizuri katika tamthilia yao inayoitwa "Msitu wa Ndendemba" nayorushwa kwenye kituo cha runinga cha Sibuka kila siku ya Jumamosi saa 6:30 mchana na ikirudiwa Jumapili kuanzia saa 2:30 asubuhi ,  akiigiza katika kikundi cha New Hope maskani yake Tandale jijini Dar es Salaam.

Kibena anadai aliachishwa shule ili kuficha yale yaliyomkuta lakini ujauzito huo uliharibika ingawa watu wanazusha kuwa msanii huyo alitoa mimba, hata hivyo Kibena amesema hatorudia makosa kwa sasa anajituliza mpaka atakapopata mchumba atakayeweza kumuoa

Sophia Abdul "Kibena" aliacha shule kisa mimba

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA