Mzee Kilomoni apigwa dundo Simba
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Klabu ya Simba leo imefanya mkutano wake wa wanachama katika ukumbi wa kisasa wa Mwl Nyerere (Mnicc) uliopo Osterbay jijini Dar es Salaam, Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah "Try Again" aliongoza mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wanachama wa klabu hiyo.
Klabu hiyo mbali ya kutangaza maazimio mbalimbali kwanza ilianza kutoa takwimu za fedha ambapo ilitangaza jumla ya shilingi Bilioni 1.3 kutumika katika usajili.
Kisha ikatangaza kumsimamisha uanachama aliyekuwa mchezaji na kiongozi wa zamani wa klabu hiyo Hamisi Kilomoni na kumvua udhamini mkuu na nafasi yake akipewa Adam Mgoyi.
Mzee Kilomoni pia ametishiwa kufukuzwa endapo asipoenda kufuta kesi aliyoifungua mahakamani, Kilomoni amesimamishwa uanachama kwa kosa la kupeleka masuala ya mpira mahakamani, pia Simba imemuongezea Prof Juma Kapuya katika Bodi ya wadhamini