Yanga yaikalisha Mlandege, Ajibu atisha

Na Mwandishi Wetu. Zanzibar

Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga SC, jana usiku waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar mchezo wa kirafiki.

Yanga iliwasili asubuhi ya jana ikitokea jijini Dar es Salaam ambapo juzi ilipokea kichapo cha bao 1-0 toka kwa masarange wa Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo mwingine wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Ibrahim Ajibu alifungua akaunti yake ya mabao akifunga bao lake la kwanza tangia ajiunge na Yanga akitokea Simba lakini pia lilikuwa bao la kwanza kwa Yanga kisha akaseti lingine la pili lililofungwa na winga Emmanuel Martin.

Yanga wanajiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao Simba SC utakaopigwa Agosti 23 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam

Emmanuel Martin, alifunga bao la pili jana

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA