WOLPER AGEUKIA MUZIKI
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Video queen wa bongofleva, Leonarda Wolper ameamua kujikita kwenye muziki wa bongofleva na sasa anatarajia kutengeneza wimbo wake mwenyewe, ambapo amedai utazungumzia mahaba.
Wolper ameyasema hayo leo alipozungumza na Mambo Uwanjani asubuhi ya leo ambapo alidai tayari ameshaanza maandalizi ya kuachia wimbo huo atakaourekodi katika studio za Jini Records zilizopo Tabata Shule.
Hata hivyo Wolper amedai si kwamba ataacha uigizaji isipokuwa ataendelea kuwa video queen kwani ndio fani iliyomtambulisha, Wolper ameanza kujipatia umaarufu mkubwa kupitia kazi zake zikiwemo filamu alizoigiza kama Lovennes