Kilomoni asema ajafutwa uanachama, na afuti kesi
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Aliyekuwa Mdhamini wa klabu ya Simba, mzee Hamisi Kilomoni amesema atambui kufutwa uanachama kama ilivyotangazwa na klabu hiyo na pia hawezi kwenda kuondoa kesi yake akiyoifungua mahakamani.
Akizungumza na mtandao huu, Kilomoni amesema yeye bado kiongozi wa bodi ya wadhamini wa klabu ya Simba na amedai maamuzi ya kumsimamisha uanachama wameyafanya wao tu ili kudanganyana na kamwe hakuna atakayeweza kumsimamisha wala kumfuta uanachama.
Kilomoni amedai hawezi kwenda kuifuta kesi aliyoifungua katika mahakama ya mkazi ya Kisutu na amesema ataendelea kuushinikiza uongozi juu ya mpango wake wa kutaka kumuuzia klabu mfanyabiashara Mohamed Dewji