Yanga na udambwidambwi wa Tshishimbi leo
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wanashuka uwanja wa Uhuru jioni ya leo kuwakaribisha Lipuli FC ya Iringa mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Mabingwa hao wametoka kufungwa na watani wao wa jadi Simba SC mabao 5-4 yaliyopatikana kwa matuta kufuatia sare tasa ya 0-0 mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Lakini licha ya Yanga kupoteza kwa matuta, wameibuka kidedea kutokana na mchezaji wao Papy Tshishimbi kupiga mpira mkubwa kiasi kwamba aliweza kuwafunika nyota wote wa Simba, Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima.
Hivyo mashabiki wa Yanga watajitokeza kwa wingi kumuona tena akifanya vitu vyake adimu mbele ya vijana wa Lipuli wanaonolewa na Seleman Matola, Lipuli nao wametamba kuonyesha soka safi kwani nao wana wachezaji mahiri kama vile ilivyo Yanga