YANGA YAPATA PIGO KUFUNGIWA KWA KIUNGO WAKE

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Mabingwa wa soka nchini Yanga wamepata pigo kufuatia kufungiwa kwa kiungo wake Pius Buswita na Shirikisho la mpira wa miguu nchini,(TFF) kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Buswita amekutwa na makosa hayo na Kamati ya Sheria, Nidhamu na Hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka nchini akiwa amesaini vilabu viwili vya Simba na Yanga.

Mchezaji huyo ambaye msimu uliopita alikuwa anaichezea Mbao ya Mwanza, ameiachia pigo klabu yake ambayo ilimsajili msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili kwa lengo la kuitumikia timu yao.

Shirikisho la soka nchini limekuwa likitoa adhabu kwa wachezaji wanaokutwa wamesaini timu mbili kwani kufanya hivyo ni kosa kubwa sana

Pius Buswita (Aliyevaa jezi ya bluu) amefungiwa na TFF

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA