HAMOSNOTA AACHIA BONGE LA SINGO

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Mwanamuziki wa kizazi kipya Hashim Momba "Hamosnota"  ambaye kwa sasa anakuja juu na wimbo wake uitwao "Pole", ameachia bonge la singo linalokwenda kwa jina la "Uwezo sina" ambao ameurekodi katika studio za Jean Records chini ya prodyuza machachari Naroh Wings.

Akizungumza na Mambo Uwanjani, Hamosnota amesema ameamua kuachia wimbo mpya kwakuwa mashabiki wake wanataka radha, anasema baada ya kuachia wimbo wa Pole ambao ulipata wafuasi wengi, sasa amekuja kivingine.

"Wimbo wangu huu tofauti na ule wa Pole ambao ulikuwa wa kutulia, lakini wimbo huu mpya unachezeka na si wa taratibu kama ule", alisema Hamosnota ambaye amewataka mashabiki wake kujiandaa na video ya wimbo huo atakairekodi hivi karibuni.

Msanii huyo amedai alikwama kutengeneza video baada ya kufuatia kufiwa na baba wa mke wake hivyo kumeweza kumfanya asimamishe shughuri zake, wimbo huo tayari ameshausambaza mitandaoni bado kwenye vituo vya redio na kwingineko

Hamosnota ametoa wimbo mpya

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA