Ishu ya kukutwa fuvu la binadamu Uwanja wa Taifa iko hivi

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Kumeibuka wasiwasi kwa mafundi wanaokarabati uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya kuliona fuvu linalodaiwa kuwa la binadamu ambalo lilifukiwa chini ya uwanja huo.

Haijajulikana kama fuvu hilo lilizikwa lini na watu gani, lakini imani za kishirikina zimetajwa, mafundi hao wa moja ya kampuni iliyopewa kandarasi ya kukarabati uwanja huo imeanza kuingia shaka.

Watani wa jadi Simba na Yanga wanatajwa kuhusika na fuvu hilo kwakuwa waliutumia uwanja huo Jumatano iliyopita walipokutana katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii ambapo Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare tasa 0-0.

Vitendo vya imani ya kishirikina vimekuwa vikilaaniwa vikali kwani vimehusisha roho za watu ikiwemo fuvu hilo la binadamu, hata hivyo vilabu vya Simba na Yanga vimegoma kuzungumzia ishu hiyo vikidai havitambui kuwepo kwa ushu hiyo kwani wao wanajihusisha na soka

Mafundi wa Uwanja wa Taifa wamelifukua fuvu la binadamu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA