Nasikia sikia, Mark Dallarz amekuja kuwashika
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Ngoma mpya ya mkali wa Hip Hop tangia kitambo, Salum Rashid A K A Mark Dallarz mwenyewe anapenda kujiita Ukuni au Cannavaro tayari imeshatoka na mashabiki wake wameanza kuchizika nayo.
Ngoma hiyo inakwenda kwa jina la "Nasikia sikia" na ameirekodi katika studio za Jini Record chini ya prodyuza anayekuja juu kwa sasa hapa mjini Naroh Wing.
Dallarz muasisi wa kundi la TBT Crew lililokuwa likimshirikisha memba KG Soon ambao walitamba na ngoma yao Segerea, amesema wimbo wake huu wa sasa :Nasikia sikia' ni bomba ile mbaya na lazima ukubalike na kushika namba moja kwenye Top Ten za radio hapa nchini.
Dallarz ambaye kwa sasa maskani yake ni Morogoro mji kasoro bahari amekuwa akionekana jijini Dar es Salaam kwa shughuri maalum kama za usambazaji wa kazi zake