Simba yaanza na kifurushi cha wiki, Okwi akamatiki

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba SC jioni ya leo wameanza vema Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Baada ya kuichakaza vibaya Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani mabao 7-0 Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Mchezo ulikuwa wa upande mmoja ambapo Simba walianza kuutawala huku viungo wake James  Kotei na Mzamiru Yassin wakicheza vizuri, Emmanuel Okwi amefunga magoli manne peke yake huku akisaidia kuseti lingine moja ambalo lilifungwa na Erasto Edward Nyoni.

Magoli mengine ya Simba yamefungwa na Juma Luizio Ndanda na Shiza Kichuya, kwa matokeo hayo Simba imekalia kiti cha uongozi wa ligi.

Matokeo mengine kama ifuatavyo. Kule mjini Mtwara katima uwanja wa Nangwanda Sijaona, Azam FC imewalaza wenyeji Ndanda FC bao 1-0, mjini Shinyanga, Mwadui imeifunga Singida United mabao 2-1 uwanja wa Mwadui Complex.

Mtibwa Sugar imeutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Manungu Complex baada ya kuilaza Stand United bao 1-0, Mbao FC imeichapa Kagera Sugar pia bao 1-0 katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Tanzania Prisons imeichakaza Njombe mji mabao 2-1 katika uwanja wa Sabasaba Njombe na Mbeya City imeilaza Majimaji bao 1-0 uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, kesho Yanga itaikaribisha Lipuli ya Iringa katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam

Emmanuel Okwi ameanza na moto Ligi Kuu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA