Simba yahofia kichapo kwa Yanga
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam.
Simba tayari wameanza kuingja hofu ya kupoteza pambano na watani wao Yanga SC litakalopigwa Jumatano ijayo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hanspoppe amewaweka kitimoto wachezaji wao kuelekea mchezo huo hasa akiamini kabisa watabweteka siku hiyo wakiamini wao ni bora kuliko wenzao.
Hanspoppe amesema kwa sasa Simba inaonekana ni timu bora kuliko Yanga hivyo wachezaji wataingia uwanjani wakiidharau Yanga na mwishowe watapoteza mchezo, amesema hata wao msimu uliopita waliifunga Yanga mabao 2-1 wakiwa hawapewi nafasi yoyote ya kushinda kutokana na kikosi cha Yanga kuwa bora.
Na ndivyo itakavyotokea Jumatano ijayo watakapocheza na Yanga ambao kwa sasa wanaonekana si lolote si chochote, Yanga wameweka kambi yao Pemba wakati Simba wapo Unguja