Okwi aanza balaa lake, apiga bonge la bao
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mabingwa wa kombe la FA, Simba SC jioni ya leo imechomoza na ushindi wa bao 1-0 mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Goli la ushindi limefungwa na Mganda, Emmanuel Okwi aliyepokea pasi murua kutoka kwa John Bocco "Adebayor", huo ni ushindi wa pili mfululizo baada ya Jumanne iliyopita kuichapa Rayon Sports bao 1-0.
Okwi alitoa pasi nzuri ambapo Mohamed Ibrahim "Mo" aliifungia Simba bao la ushindi, Simba inaendelea kukisuka kikosi chake ambapo itacheza na Ruvu Shooting kabla haijaivaa Yanga Agosti 23 mwaka huu kuwanjia Ngao ya Hisani katika Uwanja hup huo wa Taifa