TSHISHIMBI AMWAGA WINO YANGA, AENDA PEMBA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kiungo nyota wa Mbabane Swallows ya Swaziland, Papy Tshishimbi Kabamba raia wa DRC, amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC na tayari ameshawasili kisiwani Pemba kuungana na wenzake.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Yanga,Hussein Nyika amesema kuwa tayari wameshamalizana na Tshishimbi na wameshampeleka Pemba kuungana na wachezaji wenzake ambao walienda huko tangia jana wakitokea Unguja ambapo walicheza juzi na Mlandege na kushinda 2-0.
Yanga imekwenda Pemba kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya mtani wake wa jadi Simba, huo utakuwa mchezo wake wa nne kabla ya kuingia kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017/18 ikiwa kama bingwa mtetezi