KABWILI KUANZA LANGONI NA SIMBA

Na Ikram Khamees. Pemba

Kuna kila dalili mlinda mlango chipukizi wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC, Ramadhan Kabwili akaanza langoni katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao Simba mchezo utakaofanyika Jumatano ijayo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina, huenda akamuanzisha kipa huyo kwakuwa Beno Kakolanya hayupo fiti kuanza katika mchezo huo huku mlinda mlango anayemuamini kuanza kwenye mchezo huo Mcameroon, Youthe Rostand Jehu amewekewa pingamizi na klabu yake ya African Lyon na ikizingatiwa huo ni mchezo unaosimamiwa na shirikisho la soka nchini, (TFF).

Kabwili anapewa nafasi kubwa ya kuanza katika mchezo huo na huenda akavunja rekodi ya Peter Manyika Jr ambaye naye aliaminiwa kucheza mechi ya watani baada ya makipa namba moja na mbili kukosekana, Lwandamina alikuwa skimpanga Kabwili katika mechi za kirafiki

Kipa Ramadhan Kabwili ataanza langoni na Simba Jumatano ijayo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA