Msanii Viso anusurika kifo Handeni
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Vincent Patrick "Viso" amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari akiwa safarini mjini Tanga juzi Jumamosi.
Akizungumza na Mambo Uwanjani kwa njia ya simu leo, Viso amesema alipata ajali ya gari na kuumia kifuani pamoja na mgongoni, Viso amedai alipokuwa mjini Tanga ambapo ni kwao, alienda eneo moja linaloitwa Kwa Msisi na wenzake walipanda roli aina ya Fuso.
Anasema wakiwa njiani roli hilo lilishindwa kupanda kilima na kujikuta likirudi kinyumenyume na kuanguka ambapo yeye aliumia kifuani na mgongoni huku abiria wengine waliokuwemo kwenye roli hilo walivunjika mikono, miguu na viuno.
Hata hivyo amesema yeye anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu kutoka katika hospitali ya Handeni, roli hilo lilikuwa linatokea Kwa Msisi likielekea Mkata ambapo kulikuwa na gulio, kwa sasa Viso amerejea Dar es Salaam na anaendelea na matibabu, msanii huyo tayari ametambulisha wimbo wake mpya uitwao "Kipendacho roho" aliourekodi kwa prodyuza Naroh Wings