Licha ya kufungwa, Yanga yang' ara na Tshishimbi wake, apiga mpira mkubwa jana
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Yanga jana licha ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 5-4 na watani zao wa jadi Simba SC katika mchezo wa Ngao ya Jamii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, lakini imeondoka na faida kuu mbili ikiwemo nyota wake wawili kupiga mpira mkubwa ile mbaya.
Mchezo huo uliomalizika kwa sare isiyo na mabao yaani 0-0, Yanga ilionekana kuizidi Simba kwenye eneo la katikati kiasi kwamba kiungo wake James Kotei akishindwa kumpandishia mipira Mzamiru Yassin ambaye alishindwa kung' ara.
Huku Emmanuel Okwi ambaye alikuwa akitegemewa kwenye eneo la ushambuliaji naye akishindwa kufanya yale aliyozoea kuyafanya, lakini unaambiwa mtu aliyeikata umeme Simba katikati si mwingine ni Papy Kabamba Tshishimbi raia wa DRC ambaye gumzo kwa sasa hapa mjini.
Kwa upande wa ulinzi, mtu aliyemnyima raha Okwi si mwingine ni Gardiel Michael Mbaga ambaye alikuwa na kazi ya kuhakikisha anafuta makosa yote yaliyokuwa yakifanywa na Kevin Yondan, Andrew Vincent "Dante" na Juma Abdul.
Maneno yanayozagaa hapa mjini kwa sasa ni Usajili wa Bilioni 1.3 vsTshishimbi, ama kweli Mkongoman huyo anajua ile mbaya kwani Simba licha ya kutwaa ubingwa lakini bado wanamuwaza Tshishimbi na Gardiel