SIMBA KUTESTI MITAMBO NA MLANDEGE
Na Salum Fikiri Jr. Unguja
Simba SC jioni ya leo inatelemka katika Uwanja wa Amaan,Zanzibar kucheza na timu ya Mlandege mchezo wa kirafiki kujiandaa na mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao Yanga, Jumatano ijayo.
Mechi hiyo ya watani itachezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo vigogo vyote vimetoka nje ya Dar es Salaam kusaka uchawi visiwani Zanzibar, Yanga wao wapo Pemba ambapo kabla walicheza na Mlandege na kushinda mabao 2-0.
Mchezo wa leo kati ya Simba na Mlandege utatoa taswira kuelekea mpambano huo, Simba leo itashusha silaha zake zote ikiongozwa na Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, John Bocco na Shiza Kichuya na kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema leo watapata ushindi wa mabao mengi kwakuwa ameinoa vema safu yake ya ushambuliaji