MO AWAPA NGAO YA JAMII SIMBA, MAHADHI AWAAMGUSHA YANGA

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Mabingwa wa kombe la FA, Simba SC ama Wekundu wa Msimbazi usiku huu wameongeza taji lingine baada ya kutwaa Ngao ya Jamii kwa kuichapa Yanga SC kwa mikwaju ya penalti 5-4 kufuatia sare tasa ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Hiki kinakuwa kipigo cha tatu mfululizo kwa Yanga dhidi ya Simba, Ikifungwa kwa mikwaju ya penalti 4-2 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi Zanzibar pia ikaambulia tena kipigo cha mabao 2-1 mjini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo wa leo Yanga walianza vizuri kulitia msukosuko lango la Simba lakini washambuliaji wake Ibrahim Ajibu na Donald Ngoma wakishindwa kumalizia, kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi na Raphael Daudi walionekana kuwamudu viungo wa Simba.

Simba nao walikuja juu na kulisakama lango la Yanga lakini nao washambuliaji wake Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima na Laudit Mavugo nao hawakuwa imara, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafungana.

Kipindi cha pili nacho kilikuwa kigumu kwani timu hizo hazikufungana zaidi ya kushambuliana kwa zamu, mpira ulinalizika na timu hizo zikapigiana penalti tano ambapo Simba wakapata tano Yanga wakapata nne.

Waliofunga kwa upande wa Simba ni Method Mwanjali, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya na ya ushindi ilipigwa na Mohamed Ibrahim "Mo", aliyekosa ni Mohamed Hussein "Tshabalala".

Kwa upande wa Yanga waliopata ni Papy Tshishimbi, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Ibrahim Ajibu Migomba, waliokosa ni Kevin Yondani na Juma Mahadhi

Mo akishamgilia goli lake

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA