Tshishimbi awasili Pemba kuiwahi Simba
Na Ikram Khamees. Pemba
Kiungo mpya wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC, Papy Tshishimbi Kabamba raia wa DRC amewasili leo nchini akitokea nyumbani kwao DRC.
Tshishimbi moja kwa moja ameelekea kisiwani Pemba ambako Yanga imeweka kambi kujiandaa na kucheza na mtani wake wa jadi Simba Jumatano ijayo katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwania Ngao ya Jamii.
Kutua kwa kiungo huyo kunapunguza presha kwa mashabiki wa mabingwa hao wa Bara ambao jana waliichapa Chipukizi bao 1-0 bao lililofungwa na Ibrahim Ajibu mchezo ukiwa ni wa kirafiki, Tshishimbi amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mbabane Swallows ya Swaziland