Chirwa mambo safi Yanga

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Kamati ya nidhamu, sheria na haki za wachezaji ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) imemaliza utata uliokuwa ukiwaandama wachezaji wa Yanga, Obrey Chirwa raia wa Zambia na Simon Msuva ambao walisimamishwa kutokana na makosa waliyofanya msimu uliopita.

Nyota hao wawili walisimamishwa kucheza Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu baada ya kudaiwa kumsukuma mwamuzi aliochezesha mechi kati ya Yanga na Mbao FC mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara.

Msuva yeye tayari ameshaachana na Yanga ambapo amesajiliwa na Difaa El Jajida ya Morocco wakati Chirwa bado anakipiga Yanga na amekosa mechi mbili moja ikiwa ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na nyingine ya Ligi Kuu Bara.

Lakini leo hii kamati hiyo imetangaza kuwaachia huru nyota hao, kwa maana hiyo Chirwa sasa ataichezea Yanga katika mechi zijazo za Ligi Kuu Bara wakati Msuva ataitumikia timu ya taifa, Taifa Stars ambayo mwishoni mwa wiki itacheza na Botswana mchezo unaotambuliwa na Fifa

Obrey Chirwa yuko huru sasa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA