Simba na Yanga hakuna kuremba

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Watani wa jadi wa soka la Tanzania Simba SC na Yanga SC leo jioni zinaumana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwania Ngao ya Jamii, miamba hiyo inakutana kila mmoja ikiwa imetokea Visiwani Zanzibar ambako ilikwenda kuweka kambi.

Kwa upande wa Yanga, walielekea katika kisiwa cha Pemba lakini walianza kufikia Unguja ambapo walicheza mechi moja ya kirafiki na Mlandege na kushinda mabao 2-0, kisha wakaelekea Pemba ambapo pia walicheza mechi mbili za kirafiki.

Yanga ilicheza na Chipukizi na kushinda bao 1-0 kisha ikainyoa Jamhuri pia bao 1-0, itashuka uwanjani leo ikimtegemea zaidi mshambuliaji wake mpya Ibrahim Ajibu ambaye katika mechi hizo aliweza kufunga.

Simba nao walifikia Unguja ambapo wao walicheza mechi mbili za kirafiki ambapo walilazimishwa sare na Mlandege 0-0 kisha wakaichapa Gulioni mabao 5-0, Laudit Mavugo anapewa nafasi kubwa ya kuiongoza Simba kutokana na kuifungia mabao mawili Simba ilikuwa Zanzibar, ingawa kutakuwa na kivutio toka kwa Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi kwa upande wa Simba na Donald Ngoma na Amissi Tambwe kwa Yanga.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 11:00 za jioni na timu zote zinanolewa na makocha wa kigeni ambao watahakikisha wanalinda vibarua vyao, Ligi Kuu itaanza rasmi Jumamosi ya Agosti 26

Simba na Yanga wanaumana leo Uwanja wa Taifa Dar es Salaam

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA