MAYANGA ATANGAZA KIKOSI CHA STARS NA KUWARUDISHA WAKONGWE

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Salum Shaaban Mayanga, leo ametangaza majina ya wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars watakaoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na Fifa.

Katika kikosi hicho, Mayanga amewarudisha tena wakongwe Mwadini Ally na Kevin Yondan huku akimtema kipa bora wa michuano ya Cosafa Castle Cup, Said Mohamed Nduda ambaye ni majeruhi.

Kikosi kamili hiki hapa:

Makipa:

Aishi Manula (Simba SC)
Mwadini Ally (Azam FC)
Ramadhan Kabwili (Yanga SC)

Mabeki:

Gardiel Michael (Yanga SC)
Boniface Maganga (Mbao FC)
Kevin Yondan (Yanga SC)
Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).

Viungo:

Himid Mao (Azam FC)
Hamisi Abdallah (Sony Sugar ya Kenya)
Mzamiru Yassin (Simba SC)
Said Ndemla (Simba SC)
Simon Msuva (Difaa El Jadida ya Morocco)
Shiza Kichuya (Simba)
Farid Musa (Tennerife ya Hispania)
Morel Ergenes (Famalicao ya Ureno)

Washambuliaji:

Raphael Daudi (Yanga SC)
Kevin Sabato (Mtibwa Sugar)
Mbwana Samatta (KRG Genk ya Ubelgiji)
Elius Maguli (Dhofar ya Oman)

Salum Mayanga kocha wa Taifa Stars

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA