YANGA YATUA KIMAFIA, KAZI IPO KESHO
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga SC kimewasili muda huu kikitokea Pemba ambako kiliweka kambi kujiandaa na mchezo wa kesho wa kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya mtani wake wa jadi Simba katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mabingwa hao wa Bara wametua kimafia kwani hawakutaka kuzungumza na mtu yoyote na moja kwa moja waliekelekea kambini ambapo pia wamefanya siri.
Kesho Yanga itakutana na Simba katika mchezo unaotajwa utakuwa mkali na utakaotoa mshindi kwakuwa hakutakuwa na sare kwani hata zikimaliza dakika 90 bila kufungana zitapigwa penalti, Yanga itawakosa nyota wake watatu ambao ni Beno Kakolanya, Obrey Chirwa na Geofrey Mwashiuya ambao ni majeruhi huku Simba ikimkosa John Bocco "Adebayor"