Wanachama Simba wapitisha mabadiliko
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Wanachama wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam leo wamepitisha mabadiliko na sasa Simba imeingia katika mfumo mpya wa uhuzaji hisa.
Hata hivyo klabu imeridhia kubaki kumilikiwa na wanachama badala ya mwekezaji, mwekezaji ameruhusiwa kununua hisa asilimia 50 na wanachama watabakiwa na asilimia 50.
Hisa zote 50 zitauzwa kwa Bilioni 20 na nyingine zitauzwa kwa wanachama ambao wamepunguziwa bei, katika zoezi hilo mwanachama mmoja amekataa Simba kuingia kwenye mfumo huo