YANGA YAANZA KWA SARE LIGI KUU BARA
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC imeanza vibaya Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kulazimishwa sare na wageni wa ligi hiyo Lipuli FC ya Iringa kwa kufungana bao 1-1 katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Yanga leo hawakucheza kama walivyokutana na Simba na hata kiungo wake mpya Mkongoman Papy Tshishimbi hakufanya yale aliyofanya dhidi ya Simba, Seif Abdallah Kalihe alianza kuifungia Lipuli bao la kwanza katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza.
Yanga wakasawazisha dakika ya 45 kabla ya kuelekea mapumziko goli lililofungwa na Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma, hata hivyo Lipuli walimaliza wakiwa pungufu baada ya nahodha wao Asante Kwasi kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu.
Kipindi cha pili nacho hakikuwa na magoli kwani timu zote zilishambuliana kwa zamu ingawa Yanga walionekana kuutawala mchezo licha ya Lipuli kurudi nyuma na wachezaji kujiangushaangusha hovyo ili kupoteza muda, kwa matokeo hayo Yanga ina pointi moja ni sawa kama imeanza vibaya