PAZIA LA LIGI KUU BARA KUFUNGULIWA KESHO
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara linafunguliwa kesho kwa viwanja saba kutimua vumbi, katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, wenyeji Ndanda FC watawaalika wauza lambalamba wa Azam FC wakati Kagera Sugar watawakaribisha Mbao FC katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba SC wao watawakaribisha Ruvu Shooting katika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam wakati Mwadui ya Shinyanga itaawalika Singida United ya pale Singida, Mtibwa Sugar watakipiga na Stand United katika Uwanja wa Manungu.
Mji Njombe ya mkoani Njombe yenyewe itawakaribisha Prisons katika Uwanja wa Sabasaba Njombe huku Mbeya City ikiwaalika Majimaji ya Songea, ligi hiyo itaendelea tena Jumapili ambapo mabingwa watetezi Yanga SC watawakaribisha Lipuli ya Iringa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam