Shamte aja na Tanzania ya usafi
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Tangia kuingia madarakani kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, Watanzania wamekuwa wakifanya usafi kila ifikapo Jumamosi na kwa msisitizo mkubwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi imekuwa ikichukuliwa mkazo.
Msanii Shukuru Nassoro "Shamte" anayeimba muziki wa kizazi kipya ameamua kuja na wimbo unaosisitiza ufanyaji usafi, wimbo huo unaitwa "Tanzania ya Usafi" ambapo amewashirikisha wasanii wa kundi la Hisia Soul Band lenye maskani ya Temeke.
Ndani ya wimbo huo zimesikika aauti za vijana Y. Handsome na Rubians ambapo wameutendea haki wimbo huo ambapo umeanza kuteka hisia katika vituo mbalimbali vya redio pamoja na kwenye mitandao ya kijamii.
Kufanya vizuri kwa wimbo huo, kunamrudisha tena hewani Shamte ambaye siku za hivi karibuni alipotea kidogo kutokana na ubize aliokuwa nao, msanii huyo amesema ndio kwanza moto umeanza kuwaka hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani ngoma zinaanza kutoka