JENGO LA YANGA KUPIGWA MNADA KESHO

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Jengo la makao makuu ya klabu ya Yanga lililopo Jangwani mtaa wa Twiga, kesho litapigwa mnada na kampuni ya udalali ya Msolopa kuanzia saa 4:00, asubuhi.

Taarifa za kudaiwa Yanga zimeanza kusambaa leo ambapo Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi imetangaza kuidai Yanga mamilioni ya shilingi baada ya kesi iliyofunguliwa na Baraza la Ardhi la wilaya ya Temeke na Ilala.

Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amekiri kweli Yanga inadaiwa Ardhi lakini walishafanya mazungumzo na wizara na walikubaliana kulipa deni hilo, lakini anashangaa kusikia tangazo la kupigwa mnada kwa jengo lao.

Hata hivyo Mkwasa amesema suala hilo anamfikishia kaimu mwenyekiti Clement Sanga ili aweke zuio

Jengo la Yanga kupigwa mnada kesho

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA