Mbaraka Yusuf kimeeleweka Azam
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Hatimaye klabu ya Kagera Sugar imeridhia Mbaraka Yusuf kukipiga Azam FC msimu ujao baada ya kumwekea pingamizi katika shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) ambalo wameliondoa rasmi.
Afisa Habari wa Azam FC,Jaffar Idd Maganga amesema leo kuwa, Kagera Sugar wamekubali Mbaraka kukipiga Azam na hilo ni jambo jema kwao kwani tayari walishakamilisha taratibu zote za kumsaini.
Mbaraka ameitumikia Kagera Sugar kwa misimu miwili na alitambulishwa na Azam kama mchezaji mpya kitendo ambacho kiliwachefua viongozi wa Kagera Sugar na kuamua kumwekea pingamizi, lakini Azam wakaamua kukaa chini na Kagera Sugar hatimaye kulimaliza suala hilo na sasa Mbaraka ni mali ya Azam